Tukio hilo
limekuja kufuatia madai ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya
vijiji vya wilaya hizo mbili huku ukimya wa viongozi wa wilaya ukitajwa kuwa
chanzo cha kuibuka kwa mapigano hayo.
Wakiongea na wanahabari, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sirorisimba wilaya ya Butiama
mkoani Mara wamesema mgogoro huo umeanza miaka mingi iliyopita ambapo wananchi
kutoka kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda wamekuwa wakivamia wananchi wa
kijiji hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wa
wilaya hiyo.
Walisema
uvamizi wa maeneo makubwa uliofanywa hivi karibuni katika eneo hilo
umesababisha mapigano makali na kusababisha mtu mmoja kuchomwa Mshale mgongoni
na kulazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.
Mmoja wa
majeruhi aliyechomwa mshale kwenye tukio hilo na kulazwa hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Mara Hamisi Nyahanga amesema alivamiwa kwenye eneo lake la kilimo
na wananchi na kuambiwa siku zake za kuishi zimekwisha na kuamua kukimbia ndipo
alipopigwa mshale wa mgongo .
|
No comments:
Post a Comment