MATOKEO SOKA:-Manchester United sasa uso kwa uso na Liverpool katika Kombe la International Champions-Jumatatu Agosti 04,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 03, 2014

MATOKEO SOKA:-Manchester United sasa uso kwa uso na Liverpool katika Kombe la International Champions-Jumatatu Agosti 04,2014.


Umati wa mashabiki 109,00 ndani ya Michigan mjini Ann Arbor Agosti 02,2014,ambapo Manchester United imewafunga mabingwa wa Ulaya, Real Madrid mabao 3-1 katika Kombe la Kimataifa.

MANCHESTER United imewafunga mabingwa wa Ulaya, Real Madrid mabao 3-1 katika Kombe la Kimataifa Uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor, Detroit nchini Marekani hapo Jana Agosti 02,2014,usiku. 

Shujaa wa United alikuwa ni winga Ashley Young aliyefunga mabao mawili- huku bao pekee la Real likifungwa Gareth Bale.

Young alifunga bao la kwanza kwa kikosi cha Louis van Gaal dakika ya 20, kabla ya Madrid kusawazisha kwa penalti kupitia kwa Bale dakikan ya 27.

Lakini Young tena akamuinua kitini kocha Van Gaal dakika ya 37 akiunganisha vizuri krosi kumtungua kipa Iker Casillas. 

Nyota wa zamani wa United, Cristiano Ranaldo ambaye kabla ya mcheo huo alisema hajawahi kukataa kurudi timu hiyo, aliingia dakika ya 74, lakini akashindwa kuisaidia timu yake. 


.............Shaw na Tyler Blackett wakitafuta mbinu za kumpokonya mpira Ronaldo .......

Danny Welbeck akipambana na beki 'mtata' Pepe ambapo Javier Hernandez ‘Chicharito’ akawafungia Mashetani Wekundu bao la tatu dakika ya 80 mbele ya mashabiki 109,318 waliotapisha Uwanja wa Michigan.

Wachezaji wa Manchester City wakiwa wamejichokea baada ya kutolewa kwa penalti 5-4 na Olympiacos mjini Minneapolis katika Kombe la Kimataifa kufuatia safe ya 2-2.

Kipa Roberto Jimenez Gago alikuwas shujaa wa timu ya Ugiriki baada ya kucheza penalty.


Joe Allen akipongezwa na Rickie Lambert baada ya kuifungia bao la kwanza Liverpool dhidi ya AC Milan.

Nayo  Liverpool itakwenda Miami kupambana na wapinzani Manchester United Jumatatu kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya AC Milan mjini Charlotte.

Mabao ya Joe Allen na Suso yameifanya timu ya Brendan Rodgers ishinde mechi ya tatu katika Kombe la Kimataifa nchini Marekani.

Liverpool tayari ilikuwa imejihakikishia kuongoza kundi lake kufuatia kipigo cha Manchester City kwa penalti 5-4 kutoka kwa Olympiacos baada ya sare ta 2-2.


UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad