AJALI ARUSHA:-Basi la Hood lagongana uso kwa uso na Daladala…’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 03, 2014

AJALI ARUSHA:-Basi la Hood lagongana uso kwa uso na Daladala…’


Watu watano (5) wamekufa na wengine ambao idadi yao haijafahamika mara moja kujeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wanasafiria mali ya Kampuni ya Hood, lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, kugongana uso kwa uso na daladala (kifodi) inayofanya safari zake kati ya Arusha mjini hadi Tengeru katika eneo la Kilala mapema jana Agosti 02,2014, asubuhi.

Mashuhusda wa tukio hilo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likiwa katika mwendo kasi na kutaka kulipita lori la mafuta lililokuwa liko mbele yake na kusababisha kugongana na daladala hiyo na kupelekea watu watano kufa papo hapo.

Taarifa za awali zinasema kuwa, mara baada ya ajali kutokea dereva wa basi la Hood alijaribu kukimbia lakini Wananchi waliweza kumtambua na kumkamata kutokana na sare alizovaa.


Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kuwa taarifa zaidi itatolewa baada ya kujua idadi ya majeruhi na watu waliopoteza maisha kutokana na baadhi ya majeruhi kuwa na hali mbaya.

Amesema majeruhi wa tukio hilo wamepelekwa katika Hospitali ya mkoa wa huo Mount Meru.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad