MAJAABU DUNIANI:-Tazama Picha 5 za Rolf Bushholz Mjerumani aliyezuiwa kuingia Dubai akihofiwa kuwa Mchawi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 19, 2014

MAJAABU DUNIANI:-Tazama Picha 5 za Rolf Bushholz Mjerumani aliyezuiwa kuingia Dubai akihofiwa kuwa Mchawi.

Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe usoni…Mwanaume huyo kutoka Ujerumani anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyejitoboa zaidi mwili wake, Rolf Buchholz hivyo alikatazwa kuingia Dubai kutokana na sababu za kiusalama.

 Rolf alikuwa amejipanga kufanya onesho la sarakasi na kikundi chake nchini humo ambapo huonesha michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘kumeza mapanga’.

Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453 ikiwemo usoni mwake na ana pembe mbili juu ya paja la uso wake.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa ameandaliwa kufanya onyesho katika klabu moja mjini humo.

Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .

Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012 na Rolf Buchholz anatajwa kuwa mtu mwenye tattoo nyingi zaidi duniani.
....Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake.......

Alieleza wanahabari wa Press News Agency kuwa hapo awali alikuwa amekubalika lakini baadaye akarejeshwa kabla ya kufika eneo la maafisa wa usafiri ndipo akarejeshwa katika ndege iliyokuwa ikielekea mjini Instabul Uturuki.

Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.

......Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz ulivyotogwa....

Maafisa wa mgahawa huo wa Fairmont Dubai wamesema kuwa walifanya chochote kadri ya uwezo wao kumuingiza Buchholz nchini Dubai lakini hawakufua dafu.

Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.

Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad