LIGI KUU UINGEREZA 2014/2014:-Soma Matokeo ya mechi saba zilizopigwa katika viwanja tofauti Leo Agosti 16,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 16, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2014:-Soma Matokeo ya mechi saba zilizopigwa katika viwanja tofauti Leo Agosti 16,2014.


LIGI kuu soka nchini Uingereza imeanza leo (Agosti 16,2014) kwa mechi saba kupigwa katika viwanja tofauti.

Mechi ya mapema ilishuhudiwa katika dimba la Old Trafford ambapo wenyeji Manchester United chini ya kocha mpya, Mholanzi, Louis Van Gaal walilala 2-1 dhidi ya Swansea City.

Katika mechi nyingine za Jioni, Leicester City wakiwa nyumbani wamelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton.

QPR wakiwa nyumbani wamechapwa bao 1-0 na Hull City, wakati Stoke City nao wamelala 1-0 wakiwa uwanja wa nyumbani dhidi ya Aston Villa.

Katika mechi nyingine West Brom wametoka sare ya mabao 2-2 na Sunderland.
Tottenham wakiwa ugenini wameshinda bao 1-0 dhidi ya wenyeji West Ham United.

Mechi ya mwisho leo hii inaendelea baina ya Asernal dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Emirates mjini London na imemaliza dakika zake 90 kwa kutoka sare ya bao 2-1 kwa goli za Laurent Koscielny dk 45 na Aaron Ramsey dk 90.

Ligi hiyo itaendelea kesho Agosti 17,2014, ambapo washindi wa pili wa msimu uliopita, Liverpool watakuwa katika dimba lao la Anfield kuchuana na Sounthampton, wakati mabingwa Manchester City wataoneshana kazi ugenini na Newcastle United.

Jumatatu ya wiki ijayo,Agosti 18,2014,Kocha Jose Mourinho ataiongoza Chelsea kuanza na timu mpya ya Burnley.


UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad