EPL 2014/2015:-Haya hapa ndio Matokeo ya Manchester United v/s Swansea City uwanjani Old Trafford. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 16, 2014

EPL 2014/2015:-Haya hapa ndio Matokeo ya Manchester United v/s Swansea City uwanjani Old Trafford.

Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Barclays Premier League imeanza rasmi leo Agosti 16,2014, kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Manchester United dhidi ya Swansea City.

 Mchezo huo uliomalizika mapema jioni hii katika dimba la Old Trafford, United imeendelea pale pale ilipoachia msimu uliopita kwa kupoteza mechi ya kwanza kwenye dimba la nyumbani kwa kipigo cha magoli 2-1.

Swansea ndio walikuwa wa kwanza kuona nyavu za United kwenye dakika ya 28 kipindi cha kwanza kupitia Ki Sung, kabla ya Wayne Rooney kusawazisha dakika 58.

Huku United wakiwa wanatafuta goli la pili, kinda Tylor Blackett akapoteza mpira kwa Wilfred Bony na kusababisha goli la pili lilofungwa na
Sigurdsson.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Swansea 2-1 Man United.

Hiki ndio kipigo cha kwanza kwa United katika mechi ya ufunguzi wa EPL tangu mwaka 1972.




Kocha Van Gaal kulia na Msaidizi wake, Ryan Giggs kushoto wakiwa hawaamini macho yao katika mchezo huo wa Leo Agosti 16,2014.



Kikosi cha Man Utd kilikuwa; De Gea; Jones, Smalling, Blackett, Lingard/Januzaj dk24, Fletcher, Herrera/Fellaini dk67, Young, Mata, Hernandez/Nani dk46 na Rooney. 

Swansea; Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor/Tiendalli, Ki, Shelvey, Routledge, Sigurdsson, Dyer/Montero dk67 na Bony/Gomis dk77. 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad