Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC).
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
Takwimu zilizotolewa na Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa vitendo vya ukatili wa
majumbani pamoja na ubakaji vimekithiri nchini kati ya Januari na Juni, mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa
habari, jijini Dar es Salaam jana (Julai 31,2014) Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe, alisema
katika kipindi hicho, wanawake pamoja na wasichana 2,878 walibakwa na vitendo
3,633 vya ukatili dhidi yao viliripotiwa kwenye vituo vya polisi nchi nzima.
Alisema kwa mujibu wa sensa
ya watu na makazi, idadi ya watu wanaishi vijijini, lakini bado huduma za
jamii, kama vile upatikanaji wa maji, huduma za afya, shule pamoja na umeme
vijijini ni duni.
“Takwimu zinaonyesha kuwa
bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji
na vifaa vya ujenzi. Kwa mfano, katika suala la upatikanaji wa maji, makazi
3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama, ukilinganisha na makazi
1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima,” alisema.
Alisema idadi ya wananchi
11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi na kwamba, wakulima
wengi bado wanatumia jembe la mkono na kwamba, uwekezaji katika mashamba
makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa.
Mlowe alisema pia kiwango cha elimu bado
kipo chini nchini, kwani kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi, idadi ya
Watanzania waliopata elimu rasmi ni 14,495,447, kati yao 11,848323 wamehitimu
elimu ya msingi, huku wenye elimu ya chuo kikuu wakiwa 337.881 tu.
Utafiti huo umeonyesha
kumekuwapo na ongezeko la tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi, mauaji
yanayotokana na imani za kishirikina na watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na
uelewa mdogo wa wananchi juu ya haki za binadamu, pia kukosekana kwa elimu ya
haki za binadamu katika mifumo ya elimu.
No comments:
Post a Comment