Wananchi wakiangalia jiwe
lililomwangukia na kumfunika Marehemu Lucia Bahati.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
Afisa mtendaji wa Kijiji cha
Shunu Benjamin Makelo akielezea tukio hilo lilivyokuwa.
|
Mkazi wa Kijiji cha Shunu
,kata ya Nyahanga Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Lucia Bahati (25) amefariki
dunia papo hapo baada ya kuangukiwa na jiwe katika eneo lililokuwa likitumika
kutengeneza kokoto kijijini humo.
Tukio hilo limetokea jana
(Julai, 31,2014) majira ya saa nne asubuhi wakati Lucia na wenzake wakichimba kokoto katika eneo
hilo lililopo katika kitongoji cha Ikorongo ambalo liliwekwa mashine za kutengeneza
kokoto wakati wa ujenzi wa Barabara za lami wilayani Kahama.
Kwa mujibu wa Angela Alex
ambaye walikuwa wakichimba kokoto katika eneo hilo na Marehemu, jiwe hilo
lilikuwa limekaa vibaya na kwamba walikuwa wakifanya kazi kwa tahadhari kabla
ya kumuangukia mwenzake.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha
Shunu Benjamin Makelo, amesema baada ya tukio hilo, wananchi walifika kusaidia
kusogeza jiwe hilo na kuutoa mwili wa Lucia ambaye ni mzaliwa wa Ilogi wilayani
humo, akiwa tayari ameshafariki.
Makelo amesema awali baada ya
kupata taarifa za tukio hilo alipiga simu polisi ambao baadae walifika na
kuuchukua mwili wa marehemu ambao sasa umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kufuatia tukio hilo, Afisa
mtendaji wa kata ya Nyahanga William Upamba amesitisha shughuli za uchimbaji wa
kokoto katika eneo hilo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu, na ametoa siku 10
kwa wenye kokoto zao kuhakikisha wameziondoa.
No comments:
Post a Comment