KATIBA MPYA TANZANIA:-Sumaye asema ni vema Bunge la Katiba likaahirishwa kupisha uchaguzi kama Maridhiano ya pande mbili Hayatapatikana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 17, 2014

KATIBA MPYA TANZANIA:-Sumaye asema ni vema Bunge la Katiba likaahirishwa kupisha uchaguzi kama Maridhiano ya pande mbili Hayatapatikana.

WAZIRI mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema ni vema bunge la katiba linaloendelea likaahirishwa kupisha uchaguzi iwapo itaonekana kukosa maridhiano ya pande mbili ili mwisho wa siku Tanzania ipate katika ya wananchi wote.

 Sumaye amesema hayo Agosti 15,2014,jioni mkoani kigoma katika kanisa la FPCT jimbo la BIGABIRO wakati akifunga kongamano maalumu la maombi ya wiki nzima yaliyoshirikisha nchi nne kuombea aman na tulivu nchini hasa wakati huu wa mchakato wa katiba mpya.

Amesema kwa ni vema bunge likaendelea kutafuta maridhiano na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA la sivyo ni vema bunge riahirishwe kupisha uchaguzi mkuu mwakani ambao unatazamiwa na wengi kuwa chanzo cha hamasa ya pande mbili katika bunge hilo badala ya matatizo ya wananchi.


Sumaye amesema bunge linaloendelea sasa katika hali ya mgogoro na sintofahamu zinazojitokeza huku fedha ya walipa kodi ikitumia itakuwa si busara kama halitasitishwa sasa.

Akizungumzia uchaguzi ujao wa 2015,Waziri mkuu mstaafu amewaasa wananchi kuepuka kuchagua mtu kutokana na rushwa ya vitu mbalimbali badala yake waangalie mtu mwadilifu mwaminifu mcha Mungu na mchapakazi.

Amesema matokeo ya viongozi hasa kuanzia vitongoji mitaa vijiji kata jimbo na Urais wanaopatikana kwa Rushwa hawana uchungu wa moja kwa moja na matatizo ya huduma za wananch kwasababu hutumia nguvu nyingi kusaka rushwa nakuhujumu mali za nchi kufidia fedha walizotumia katika uchaguzi.

Awali katika taarifa yake kwa mgeni rasmi Katibu wa Jimbo hilo David Nkone amesema utulivu amani na usalama wa Tanzania utategemea na upatikanaji wa viongozi waadilifu wanaomcha Mungu wazalendo wa Taifa wapinga rushwa na udhalimu.

Habari/Picha Na:-Jacob Ruviro-Kigoma.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad