UCHAGUZI CHADEMA:-Huu ndio Uongozi uliochaguliwa wa Chama na Mabaraza ya (CHADEMA) wilaya ya Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 17, 2014

UCHAGUZI CHADEMA:-Huu ndio Uongozi uliochaguliwa wa Chama na Mabaraza ya (CHADEMA) wilaya ya Ngara mkoani Kagera.


Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA wilaya ya Ngara( BAVICHA ) Bw. Nestory Mashishanga,katikati ni Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ,Bw.Stanford Kennedy Festo,sambamba na Wanachama John Simon Malanilo na kulia ni Mke wa Malanilo Bi. Juliana Mbowe.

Picha Na:- Maktaba yetu.
Dr. Peter Bujari.


Kushoto ni  Bi.Elda Brighton Muhimbiza, Dk. Gresmus Ssebuyoya na kulia ni Bi.Magdalena Ntazimila.

UCHAGUZI wa viongozi wa Chama na Mabaraza ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa wilaya Ngara mkoani Kagera umefanyika siku ya Ijumaa tarehe 15/08/2014 katika ukumbi wa Paradise mjini Ngara.
 
Uchaguzi huo ulianza kwa kuchagua Mabaraza ya wilaya ambapo Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza hayo walichaguliwa. 

Na yafuatayo ni Mabaraza hayo na walioshinda nafasi kwenye Mabaraza hayo.

BARAZA LA WAZEE WILAYA.

Mwenyekiti: Bw.Yustus Nyabenda Nyakubaho

Katibu: Bw.Emmanuel S. Kashaza

BARAZA LA VIJANA (BAVICHA) WILAYA.
 
Mwenyekiti: Bw.Nestory Mashishanga

Katibu:Bw. Abel Salmon Bahomoka

BARAZA LA WANAWAKE(BAWACHA) WILAYA.
 
Mwenyekiti: Bi.Catheline B. Frenk

Katibu:Bi. Elida B. Muhimbiza
 
Aidha alichaguliwa Muwakirishi wa mkutano mkuu ambapo aliyeshinda nafasi hiyo ni JOHAKIM R. DEDAN.

MTUNZA HAZINA WA WILAYA.
 
Bw.Donard Obed

KATIBU MWENEZI WA WILAYA.
 
Bw.Wilson Kakoko

MWENYEKITI WA WILAYA.
 
Bw.Kennedy Staphord Festo.

WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI WILAYA.
 
Dr. Peter Bujari

Bw.Juventus Juvenary

Dr. Gresmus Sebuyoya

Bw.Kadaga Kabudidi Kafuku

Aidha nafasi ya katibu wa wilaya haikutangazwa moja kwa moja maana mgombea wa nafasi hiyo alishinda nafasi mbili tofauti hivyo maamuzi ya nani awe katibu hayajatolewa rasmi.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad