KAGAME CUP 2014:-Mabingwa wa Tanzania bara AZAM FC Nje kwa Mikwaju ya Penati dhidi ya EL MERREIKH. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 20, 2014

KAGAME CUP 2014:-Mabingwa wa Tanzania bara AZAM FC Nje kwa Mikwaju ya Penati dhidi ya EL MERREIKH.


Kipa Salim Magoola akiwa amebebwa baada ya kupangua penalti ya Leonel Saint-Preux.

Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, Leo hii Agosti 20,2014,wametupwa nje ya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup2014, huko Kigali, Rwanda baada kutolewa kwa Mikwaju ya Penati 4-3 na El Merreikh ya Sudan kufuatia Sare ya 0-0.

Mechi hi ilikuwa ni ya Robo Fainali na sasa El Merreikh imesonga Nusu Fainali ambapo watacheza na Mshindi kati ya KCC ya Uganda na Atlabara ya South Sudan zinazokutana baadae hii Leo.

Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Klabu za Rwanda, Polisi na APR, ambazo nazo zilishinda Mechi zao za Robo Fainali kwa Mikwaju ya Penati hapo Jana Agosti 19,2014.


.........Leonel akisiktika baada ya kukosa penalty.......

Kwenye Tombola ya Penati hii Leo, Azam FC walifunga Penati 3 zilizopigwa na Aggrey Morris, Didier Kavumbagu na Erasto Nyoni na waliokosa ni Shomari Kapombe na Lionel Saint.

El Merreikh walifunga Penati 4 kupitia Allan Wanga, Majid, Aiman Said na Gafa Hussein huku Elbasha Ahmed akikosa.


Azam FC sasa inarejea Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC, Septemba 13 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Marreikh itasubiri mshindi kati ya KCC ya Uganda na Atlabara ya Sudan Kusini.

Hii ni mara ya pili Azam FC kucheza Kombe la Kagame, mara ya kwanza mwaka 2012 ambao iliingia Fainali na kufungwa Yanga SC mabao 2-0. 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad