RATIBA LIGI KUU VODACOM 2014/2014:-Icheki hapa Mechi za Kwanza Septemba 20,2014 SIMBA v COASTAL TAIFA, YANGA v MTIBWA MORO huku YANGA v SIMBA, OKTOBA 12,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 20, 2014

RATIBA LIGI KUU VODACOM 2014/2014:-Icheki hapa Mechi za Kwanza Septemba 20,2014 SIMBA v COASTAL TAIFA, YANGA v MTIBWA MORO huku YANGA v SIMBA, OKTOBA 12,2014.

Shirikisho la soka la Tanzania TFF Leo Agosti 20,2014, imetoa Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa Msimu mpya wa 2014/15 na Mechi za kwanza kuchezwa Jumamosi Septemba 20,2014.

 Ratiba hiyo, iliyosambazwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, Usajili wa Dirisha Dogo kati ya Novemba 15 na Desemba 15, ushiriki wa Klabu za Azam FC na Yanga kwenye Mashindano ya CAF ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).

Kwa mujibu wa Wambura, mechi zitachezwa Wikiendi tu ili kuongeza msisimko na kuwapa fursa Washabiki wengi zaidi kuhudhuria na katikati ya Wiki kuachwa wazi kwa ajili ya Mechi za Kombe la FA (Federation Cup).

Vilevile kutakuwa na Mechi kwenye Boxing Day na Siku ya Mwaka Mpya.

Ile Dabi inayongojewa kwa hamu Nchi nzima, Dabi ya Kariakoo, kati ya Yanga na Simba, itachezwa Oktoba 12,2014 na Marudiano ni Februari 8,2015.

Ligi itamalizika rasmi Tarehe 18 Aprili 2015.

LIGI KUU VODACOM 2014/2015.

RATIBA-Mechi za Ufunguzi

Septemba 20,2014.

Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]

Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]

Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]

Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]

Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]

Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]

Septemba 21,2014.

Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad