AJALI:-Tazama Lori la Mafuta Laanguka huku Wananchi wagombania Kuchota Mafuta. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 14, 2014

AJALI:-Tazama Lori la Mafuta Laanguka huku Wananchi wagombania Kuchota Mafuta.

Muonekano wa Lori la mafuta baada ya kuanguka…ambapo GARI hilo lenye namba T748 ABJ lililokuwa limebeba mafuta ya diseli kutoka Dar es Salaam kwenda Singida, limeanguka leo Agosti 14,2014, asubuhi na kusababisha foleni ndefu maeneo ya Kimara-Darajani jijini Dar es Salaam.

 Dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja la Juma, alikimbizwa hospitali.  Gari hilo lilikuwa na lita 34,000 za mafuta, mali ya Nassor Filling Station ya jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo wananchi wa maeneo hayo, badala ya kutoa msaada, walianza kuiba mafuta hayo kabla ya kutawanywa na polisi waliofyatua mabomu ya kutoa machozi na juhudi za kulitoa barabarani zikaanza mara moja.


Kazi ya kuhamisha mafuta kutoka kwenye gari lililoanguka kwenda jingine ikifanyika.


Polisi wakipakia madumu ya mafuta waliyoyakamata kutoka kwa wananchi.

Gari la zimamoto likiwa eneo la tukio.

Foleni iliyosababishwa na ajali hiyo eneo la Kimara, Dar.



Polisi wakitafuta mafuta yaliyoibiwa katika moja ya maduka ya jirani.

Wananchi wakiwa pembeni baada ya kufyatuliwa mabomu ya machozi.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad