UJIRANI MWEMA:-Tanzania yashauriwa kuboresha miundombinu ya reli ya kati na Barabara kwakuwa Burundi inategemea mkoa wa Kigoma kibiashara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 14, 2014

UJIRANI MWEMA:-Tanzania yashauriwa kuboresha miundombinu ya reli ya kati na Barabara kwakuwa Burundi inategemea mkoa wa Kigoma kibiashara.

Ni Viongozi  mbalimbali katika mkutano wao wa ujirani mwema baina ya Serikali ya mikoa ya mipakani toka nchi ya  Burundi na Kigoma, Tanzania wakijadili mambo mbalimbali hasa  Ulinzi , Usalama na Mahusiano ya  Kibiashara ambapo Burundi wameshauri Tanzania kuboresha miundombinu ya Reli ya kati na barabara kwa kuwa Burundi inategemea bandari za Dar es Salaam na Mkoa wa Kigoma kibiashara.Picha Na:-Mdau wetu Jacob Luviro-Kigoma.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanali mstaafu Issa Machibya (aliyesimama) pamoja na mambo mengine ,amesisitiza umuhimu wa nchi hizi (Kigoma,Tanzania na Burundi) kuboresha ulinzi wa mipaka ili kupunguza uwezekano wa mwingiliano wa waharifu na wahamiaji haramu.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa LUYIGI nchini Burundi, Bw Nshimirimana Siriyako ameipongeza Tanzania kwa hatua ya kuendesha oparesheni ondoa wahamiaji haramu ambayo amesema kuwa ilifanya wakimbizi haramu kurejea nchini kwao.


Baadhi ya waandishi wa Vyombo mbalimbali walipata fursa ya kuhudhuria Mkutano huo wa Viongozi wa Chama na Serikali kutoka Burundi na Tanzania hasa Mkoani Kigoma.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad