MBUNGE wa Tabora mjini (CCM), Ismail Aden Rage (pichani) na wenzake wanne
wamenusurika kifo baada ya kupata ajali na gari lao walilokuwa wakisafiria
kutoka Tabaora kwenda Dodoma eneo la Chigongwe mkoani Dodoma leo(Agost 04,2014).
Ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa gari walilokuwemo kujaribu
kulikwepa lori lililokuwa mbele yao na kupinduka.
Rage alikuwa anaelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge Maalum
la Katiba vinavyoanza kesho.
Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa
Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini
Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
No comments:
Post a Comment