Kipara ni
kitu ambacho kinawapata watu wengi walioko sehemu mbalimbali duniani.
Takwimu
zinaonyesha kuwa takriban asilimia 50 ya wanaume kwa nyakati tofauti maishani
mwao hujikuta wanapata kipara.
Kwa wanaume,
mara chache kipara, kinaweza kuanza mapema kati ya umri wa miaka 14 na 20,
lakini wanaume walio wengi hupata kati ya umri wa miaka 30 na 60.
Wanaume
wanaopata kipara huanza kuona nywele zikipungua kichwani hatua kwa hatua,
kuanzia upande wa mbele au katikati ya kichwa na hatimaye sehemu hiyo huwa
haina nywele kabisa.
Ingawa
kimsingi kipara hufikiriwa kuwa ni tatizo la kawaida kwa wanaume, wanawake pia
wanaweza kukabiliwa na tatizo hili.
Inasemekana kuwa karibu asilimia 40 ya
wanawake nchini Marekani, kutokana na sababu mbalimbali wana tatizo la kipara
au kunyonyoka nywele kichwani.
Kila unywele
huota na kukua katika kifuko cha nywele kiitwacho kinyweleo kilichoko kwenye
ngozi.
Chini ya
kila kinyweleo kuna kituta ambacho hushikilia unywele na kituta hiki hujulikana
kama foliko ya nywele.
Katika hali
ya kawaida wastani wa nywele 50 hadi 100 huchomoka kila siku kutoka katika
vifuko vyake katika ngozi ya kichwani na kuanguka chini.
Jambo hili
linaweza kugunduliwa kwa urahisi kwa kuona nywele kwenye vitana, chanuo au
foronya tunazotumia wakati wa kulala.
Nywele
zinapochomoka kwa wingi kuliko kawaida kila siku au zisipoota na kukua ili
kuziba pengo la nywele zilizotoka, baada ya muda mtu huwa na kipara. Wakati
mwingine nywele hupungua bila kutoka kichwani.
Hali hii
inaweza kusababishwa na kupungua kwa unene wa unywele au kutofautiana kwa kasi
ya kukua kwa nywele.
Ingawa
chanzo hasa cha upara hakifahamiki vizuri, wanasayansi wanasema kuwa kukosekana
kwa usawaziko sawia wa homoni ya kiume ya androjeni aina ya dihydrotestosterone
(DHT) mwilini, ni moja ya vyanzo vya tatizo hili.
Homoni hii
inapoongezeka mwilini hasa katika ngozi ya kichwa, husababisha mgandamizo wa
ngozi ya katikati ya kichwa na kuathiri foliko za nywele kwa kuzifanya ndogo
kiasi kwamba zinapoteza taratibu uwezo wake wa kutokeza nywele mpya.
No comments:
Post a Comment