Wakazi wa
kijiji cha Uchunga wakiwa katika eneo la tukio leo…Wafanyabiashara watatu
wamepoteza maisha na wengine 46 wamejeruhiwa vibaya.
|
Watu 3 wamekufa na wengine zaidi ya 47 wamejeruhiwa baada ya gari
walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani kupinduka wilayani Kishapu Mkoani
Shinyang'a.
Ajari hiyo imetokea asubuhi katika eneo la uchunga wilayani humo
baada ya gari hilo haina ya fuso namba T 680 ARL kuacha njia na kupinduka.
Chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi na derava wa gari hilo
aliyetambulika kwa jina la Shija Ngassa amekimbia baada ya ajari
hiyo.
Ajari hiyo ya fuso imesababisha vifo vya watu watatu ambapo moja
ametambulika kwa jina la Difa Shimo mili ya marehemu imehifadhiwa
kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyang'a.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyang'a kamishina msaidizi wa polisi
Jastus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo.
Kamugisha amesema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
pamoja na kumsaka dereva wa gari hilo sanajali na kutoa onyo kwa wafanya
biashara wa minadani kuacha kupanda magari ya mizigo.
No comments:
Post a Comment