MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI:-Ukweli Bado Unatafutwa….SOMA HAPA..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 26, 2014

MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI:-Ukweli Bado Unatafutwa….SOMA HAPA..’’

NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kchwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa.


Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.

TAARIFA FUPI.

Kwenye mitandao ya kijamii, picha hizo ziliambatana na maelezo mafupi sana kwa chini yakisomeka hivi:-“Baada ya madoctor (madaktari) wa Bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliyefumaniwa huko Mwanza hatimaye wamefanikiwa kumtoa shoka kichwani na hali yake bado mbaya, yuko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) kwa uangalizi zaidi. Mke wa mtu sumu!”

MAZINGIRA YA PICHA.

Kwenye baadhi ya picha, mwanaume huyo anaonekana ana nywele ndefu kidogo na mustachi ulionona. 

Picha nyingine zinamuonea akiwa na kipara nusu kichwa baada ya kunyolewa nywele ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kulitoa shoka hilo lililozama ndani sana.

MAZINGIRA YA HOSPITALI.

Baadhi ya watu waliochangia kwenye mitandao ya kijamii walisema tukio hilo lilitokea nje ya Tanzania. 

Walisema ingekuwa Bongo lazima vyombo vya habari vingeandika lakini hata hivyo, mazingira ya chumba cha upasuaji alicholazwa mwanaume huyo yalionesha ni Tanzania.


.....Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani......

KWA NINI NI TANZANIA?

Ni Tanzania kwa sababu, picha zinamuonesha mwanaume huyo akiwa kwenye kitanda cha chumba cha upasuaji akiwa amefunikwa shuka yenye maandishi yanayosomeka kwa kifupi MSD.

MSD ni kifupi cha maneno Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa). 

Mbali na kugawa dawa katika hospitali za serikali nchini, pia MSD inatoa mashuka yenye nembo hiyo kwa ajli ya kujifunika wagonjwa mahospitalini.

RPC ASHTUKA.

Ili kupata ukweli wa madai hayo kwamba mwanaume huyo alikutwa na mkasa huo mkoani Mwanza na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Risasi Jumamosi liliingia kazini kufuatilia tukio hilo kwa kuzungumza na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime na kumuuliza kama ana ishu hiyo mezani kwake.

“Mh! Hivi nyiye mnajua kama mitandao siku hizi imezua balaa kubwa sana? Hivi tukio kama hilo, mwanaume apigwe shoka mpaka kuzama kichwani, alazwe Bugando Hospital mimi nisijue?

“Hakuna kitu kama hicho.

Hayo ni mambo ya mitandao tu, sijui wametoa wapi? Halafu si umeona hata maelezo hayajitoshelezi? Mimi mkoa wangu upo shwari kabisa mpaka hivi ninavyoongea na wewe,” alisema Afande Fuime kwa sauti iliyoashiria kushtuka.


........Shoka likiwa limetolewa na madaktari wa upasuaji...........

....Picha ya X-Ray shoka lilivyoingia Pichani......


DAKTARI BUGANDO AONGEA.

Ili kuchimba zaidi, Risasi Jumamosi lilimtuma paparazi wake aliye Mwanza, Mashaka Bartazal ambaye alikwenda hadi Hospitali ya Rufaa, Bugando na kuzungumza na daktari mmoja anayefanya kazi kwenye kitengo cha upasuaji ambapo alisema:-“Ni kweli tunapokea watu wenye matukio ya kutisha lakini mwanaume aliyepigwa shoka mpaka likazama kichwani hatujampokea,” alisema daktari huyo akiomba asitajwe jina gazetini kwani si msemaji wa hospitali hiyo. 

UKIO LAHAMISHIWA KAHAMA.

Katika hali iliyozidi kuibua maswali, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi wetu wa Mwanza walisema wamesikia mwanaume huyo alikumbwa na balaa hilo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

RISASI JUMAMOSI KAHAMA

Kwa sababu Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa Bongo ina waandishi nchi nzima, ilimwagiza mwandishi wake aishiye Kahama kulisaka tukio hilo na kutoa ripoti Makao Makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar ambapo alifanya hivyo kwa kuomba apewe saa mbili tu kufuatilia.

Baada ya saa mbili kupita, mwandishi wetu alitoa ripoti makao makuu kwamba, hakuna mwanaume aliyelazwa kwenye hospitali yoyote ya wilayani Kahama wala mkoa huo kwa kupigwa shoka la kichwani.

MASWALI YA MSINGI

Bado jamii imebaki na maswali kadhaa ya kujiuliza. Kwamba, kama ni tukio la Tanzania, hiyo sehemu aliyolazwa mtu huyo hakuna jeshi la polisi? Kwa sababu polisi ndiyo wanahusika na kupewa taarifa za matukio kama hayo na kuyatangaza.

Pili, jamii inauliza kwamba, inawezekana mwanaume huyo baada ya tukio hakupitia au kupitishwa polisi kwa ajili ya kupewa Police Form No. 3 (PF3)?

Kama ni hivyo, hospitali walimpokeaje mtu wa hivyo hasa ikizingatiwa kuwa, hali yake ilionekana ni mbaya kwani hata picha ya X-Ray ilionesha shoka hilo lilizama kiasi cha kama inchi sita kwenda ndani na kubakiza kidogo kutokea upande wa kulia wa kichwa.

Habari Na:-GPL.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad