Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Nyamahwa ,kata ya
Nyakisasa wilayani Ngara mkoani Kagera ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito
kichwani na watu wasiofahamika,kisha
mwili wake kuutelekeza karibu na Ofisi
ya kijiji hicho.
Kaimu Afisa tarafa ya Rulenge, Bw
Elick Eliazari amemtaja
afisa huyo kuwa ni Andrew Mwakuye
(54) na kwamba alihamishiwa Kijijini hapo akitokea kijiji cha Kanazi miezi sita
iliyopita.
Bw
Eliazari amesema , tukio hilo
limetokea Usiku wa kuamkia Julai 22,2014 na mwili wake kuonekana
asubuhi huku wauwaji hao wanadaiwa
kutochukuwa fedha elfu 27 alizokuwa nazo
Marehemu pamoja na simu yake mkononi.
Aidha Mganga
mkuu wa hospital ya Rulenge ,wilayani Ngara
ambaye amefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu, Padre Frorence
Muchunguzi amesema kuwa Marehemu alipigwa na kitu kizito
kichwani na kupelekea kuvuja damu nyingi
na kupoteza maisha.
Katika tukio
Jingine,Mtoto mmoja aliyejulikana kwa
jina la Scovia Stafford mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa kitongoji cha Nyakariba B, kata
ya Kasulo wilayani humo, ameuwa baada ya kuchomwa mkuki ubavuni
na watu wasiojulikana.
Akizungumza
na Radio Kwizera FM, Baba wa mtoto huyo Bw. Stafford Patrisi amesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 20,2014, majira ya
saa nne usiku ambapo alirudi kutoka sokoni na alipofika nyumbani majira
ya saa 4 usiku alikuta nyumba imeungua
na mtoto wake amefariki.
Bw. Patrisi amevitaja vitu vilivyougulia ndani ya nyumba
kuwa ni gunia mbili za mahindi , gunia
moja la maharage, pesa taslimu shilingi
elfu 40 pamoja na vyombo na nguo ambapo ametaja thamani ya vitu hivyo
kuwa ni shilingi laki mbili na elfu kumi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyakariba B, Bw. Damiani Joseph
amesema chanzo cha tukio ni
mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji
wa kitongoji hicho uliodumu
kwa takribani wiki mbili zilizopita.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara ,Bw Abeli Mtagwa amesema Jeshi hilo
linawasaka wahusika wa Matukio hayo ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria na kuiomba Jamii kutoa ushirikiano ili kupunguza vitendo hivyo vya Mauaji.
Habari Na:-Radio
Kwizera-Ngara.
No comments:
Post a Comment