Utakumbuka
Julai 18,2014,Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Jafari Kasisiko (katikati) Katibu wa Mkoa CHADEMA, Msafiri
Wamalwa (kushoto), Katibu wa BAWATA Bi. Malunga Simba walitangaza
uamuzi wao wa kujitoa CHADEMA mbele ya waandishi wa habari Mjini Kigoma ikiwa ni
pamoja na nafasi zao
na uanachama wa chama hicho na kuachia nyadhifa zao baada ya kuona kuwa CHADEMA
kimepoteza sifa ya kuwa chama cha kidemokrasia na kuwa chama cha kibabe.
|
Baada ya
kujiuzulu uongozi na uanachama wa Chadema, Mzee Kasisiko alisema anajiunga na
chama kipya cha siasa cha Allience for Change and Transparency, ACT,
lakini wenzake hawakuzungumzia kama kuna chama wanachohamia ingawa Msafiri
Wamalwa alisema atatafuta chama makini.
|
No comments:
Post a Comment