Kamanda wa
Polisi mkoa wa Dodoma David Misime - SACP.
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la
Polisi Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na
EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam
liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya
kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME –
SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira ya saa 03:00 alfajiri
katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya
Kongwa.
Kamanda
MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o MWAKABUNGU
ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI D/O BUKUKU,
Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na mkazi wa Tabata – Dar es
Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O
CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20, Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es
Salaam yeye ana michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao
zinaendelea vizuri.
Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu
walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo,
BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye
tamasha la Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na
kutafuta gari lililowagonga.
|
No comments:
Post a Comment