DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO:-Tazama Picha 11 za Ujenzi wake umefikia asilimia kubwa ya kukamilika November 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 28, 2014

DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO:-Tazama Picha 11 za Ujenzi wake umefikia asilimia kubwa ya kukamilika November 2014.


Ni daraja jipya linalojengwa katika mto Ruvubu/Kagera.... Daraja hili linaunganisha nchi za Tanzania na Rwanda , eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.....Daraja hilo litakalokuwa na urefu wa kilometa 2 na upana wa meta 10.5 linajengwa kwa gharama ya Yeni za Kijapani bilioni 2.9 na kila nchi (Tanzania na Rwanda) zinachangia fedha za Japani Yeni bilioni 1.4 kila nchi mpaka daraja kukamilika ujenzi wake mwezi Novemba 2014. 
Kwa upande wa Tanzania mradi wote (Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha na daraja) umefadhiliwa na Serikali ya Japani kwa gharama ya fedha za Japani Yeni bilioni 1.8 na unajengwa na Kampuni ya Kijapani iitwayo DAIHO COOPERATION ambapo ujenzi wake umefikia asilimia kubwa ya kukamilika.
...Hivi ndivyo ujenzi unavyoonekana kwa sasa katika ...Mradi huo unaotekelezwa unataraji kukamilika kwa muda uliopangwa ambapo ulianza  Machi,02, 2012 na unatarajia kukamilika Novemba,15, 2014.
Ni muonekano wa barabara ya kupitia magari ilivyokamilika kuelekea kuvuka daraja hilo la Rusumo  na mara baada ya ujenzi wa Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha na daraja la kimataifa kukamilika mpaka wa Rusumo utaanza kufanya kazi kwa masaa 24 kutoka 16 ya sasa.
………..Daraja la sasa Linavyoonekana kwa picha ya Mbali……..
Pichani ni mdau wa Mwanawamakonda Blog akipozi na camera yetu akiwa kwenye daraja la sasa la mto Ruvubu/Kagera eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera na kulia juu kwake ni Daraja jipya na la kisasa katika eneo hilo likiwa linaendelea kujengwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad