UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL:- Watu kadhaa Wajeruhiwa katika Mapigano ya Polisi na Raia wanaopinga kuwepo kwa Fainali hizo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 13, 2014

UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL:- Watu kadhaa Wajeruhiwa katika Mapigano ya Polisi na Raia wanaopinga kuwepo kwa Fainali hizo.


Kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, Jiji la Sao Paulo kwa mara nyingine zimeibuka vurugu zilizosababisha watu kadhaa kujeruhiwa.Polisi walilipua mabomu ya machozi na kupambana vikali na Mashabiki maeneo ya kituo cha Caaro.. Demonstrators push over a police car during a protest demanding better public services and against the money spent on the World Cup soccer tournament in Belo Horizonte, Brazil, Thursday, June, 12, 2014.



 Police clashed with anti-World-Cup protesters who were trying to block a road near the main highway leading to the stadium that hosts the opening match to the tournament.


A masked man throws a stone towards riot policemen during a protest by people demanding better public services and against the money spent on the World Cup soccer tournament in Sao Paulo, Brazil, Thursday, June 12, 2014.


 Serikali ya Brazil imetumia dola billioni 11.5 kutayarisha mashindano haya yatakayo fanyika kwa mwezi mmoja kwa kujenga na  kuviboresha viwanja katika miji kumi na miwili ikishirikisha  timu 32 .

Waandamanaji wameandamana June 12,2014, wakiendelea kuikosoa serikali kwa jinsi ilivyotumia pesa vibaya badala ya kushughulikia mambo mengine muhimu.



 Mashindano hayo yameanza June 12,2014 kwa sherehe za ufunguzi  huko Sao Paulo kabla ya Brazil kupambana na Croatia.

Timu hii  wenyeji  inajaribu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita na mara ya kwanza tangu 2002.



Waandamanaji ambao walisababisha vurugu kubwa wakati wa kombe la mabara , Confederations Cup, mwaka jana (2013) wameapa kuandamana katika uwanja wa Sao Paulo.









Members of the media film riot policemen during a protest against the 2014 World Cup in Sao Paulo June 12, 2014






Jioni ya leo(13.06.2014) Simba wa nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati Mabingwa watetezi Hispania inaanza kampeni ya kulitetea na kulirejesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad