TANZIA:-A angukiwa na Kichuguu na kufariki papo hapo ''ni Mkazi wa kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 13, 2014

TANZIA:-A angukiwa na Kichuguu na kufariki papo hapo ''ni Mkazi wa kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera Raulian Ladislaus mwenye umri wa Miaka 40, ukiwa umeangukiwa na Kichuguu na kufariki papo hapo June 12,2014,mchana wakati akichimba kichuguu hicho kwa lengo la kuangamiza mchwa waliokuwa wakiharibu miwa yake aliyoilima  karibu kichuguu hicho.

Tukio hilo limetokea  majira ya saa 4 asubuhi wakati Marehemu akichimba kichuguu hicho ili kukihamisha kwa lengo la kusalimisha ekari moja ya Miwa iliyokuwa karibu na kichuguu hicho kabla ya kuangukiwa na kukandamizwa na Kichuguu hicho kifuani.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Uganzo walishirikiana kuchimba kichuguu hicho kwa lengo la kumtoa marehemu ambaye alizikwa jana June 12, 2014,Jioni Nyumbani Kwake.. ‘’Mungu ailaze mahali pema peponi.... Amina..’’

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad