SIKU YA MTOTO AFRICA 2014:- Serikali wilayani Ngara mkoani Kagera yatakiwa ihakikishe inawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wanaobainika kuhusika na vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watoto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 17, 2014

SIKU YA MTOTO AFRICA 2014:- Serikali wilayani Ngara mkoani Kagera yatakiwa ihakikishe inawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wanaobainika kuhusika na vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watoto.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto wa Afrika June 16,2014,yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Kabanga,wilayani Ngara mkoani Kagera..inasema ELIMU NDIO MADAI YA MSINGI ..’’

Akisoma risala kwa niaba ya watoto wenzake, Mtoto Elina Pius ameitaka serikali ihakikishe ulinzi dhidi ya vitendo vya ubakaji na watu wanaowabebesha ujauzito watoto na kusababisha kuwaharibia malengo ya kielimu na maisha pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya ubakaji na udhalilishaji mwingine kwa watoto.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw John Shimilimana alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo na amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwakatisha masomo watoto wao na kuwatumikisha kazi ngumu kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka Haki za Watoto

Amesema vitendo vya kuwatorosha wanafunzi na kwenda kufanya kazi za ndani na biashara ndogondogo kwenye mikoa mbalimbali ni miongoni mwa sababu za watoto wengi kuteswa na kufanyiwa ukatili na waajiri wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad