KOMBE LA DUNIA 2014:Argentina ,Ufaransa wang’ara vyema huku Germany v Portugal,Iran v Nigeria na Ghana v United States kupambana June 16, 2014..Nani kuibuka mkali..?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 16, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:Argentina ,Ufaransa wang’ara vyema huku Germany v Portugal,Iran v Nigeria na Ghana v United States kupambana June 16, 2014..Nani kuibuka mkali..??

Kikosi cha timu ya Taifa ya ARGENTINA imeanza vyema Kombe la Dunia baada ya June 16, 2014, usiku wa alfajiri  kuilaza Bosnia-Herzegovina mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi Kombe la Dunia Uwanja wa Maracana mjini  Rio de Janeiro, Brazil.


Shukrani kwake Mwanasoka bora wa zamani wa dunia, mshambuliaji wa Barcelona ya Hispania, Lionel Messi aliyefunga bao la pili la Argentina dakika ya 65 akimalizia pasi ya Gonzalo Higuain.
  
Sead Kolasinac aijifunga dakika ya tatu katika harakati za kuokoa kuipatia Argentina bao la kwanza kabla ya Vedad Ibisevic kutumia pasi ya Senad Lulic kuisawazishia Bosnia dakika ya 84.

Lionel Messi akishangilia bao la pili aliloifungia Argentina usiku huu katika ushindi wa 2-1…Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Argentina sasa anakuwa amefikisha magoli 39 katika mechi 87 internationals.




 


 



SHERIA ya teknolojia langoni hatimaye June 15, 2014 imetumika kikamilifu kumaliza utata wa bao ,kwa Timu ya Taifa ya Ufaransa ikiitandika mabao 3-0 Honduras katika mchezo wa Kundi E Kombe la Dunia. Karim Benzema amefunga mabao mawili mjini Porto Alegre dakika za 45 kwa penalti na 72, wakati bao lingine Noel Valladares alijifunga dakika ya 48 na kulazimika sheria ya teknolojia kwenye mstari wa goli kutumika ili kuhakikisha kama lilikuwa bao halali.

Wilson Palacios wa Honduras alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu baada ya kumsukuma Paul Pogba kwenye boksi na Benzema akafungwa kwa penalti.

As It Stood Table

Position Team Played Goal Difference Points
1 Brazil 1 2 3
2 Mexico 1 1 3
3 Cameroon 1 -1 0
4 Croatia 1 -2 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Netherlands 1 4 3
2 Chile 1 2 3
3 Australia 1 -2 0
4 Spain 1 -4 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Colombia 1 3 3
2 Ivory Coast 1 1 3
3 Japan 1 -1 0
4 Greece 1 -3 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Costa Rica 1 2 3
2 Italy 1 1 3
3 England 1 -1 0
4 Uruguay 1 -2 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 France 1 3 3
2 Switzerland 1 1 3
3 Ecuador 1 -1 0
4 Honduras 1 -3 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Argentina 0 0 0
2 Bos-Herce 0 0 0
3 Iran 0 0 0
4 Nigeria 0 0 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Germany 0 0 0
2 Portugal 0 0 0
3 Ghana 0 0 0
4 USA 0 0 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Belgium 0 0 0
2 Algeria 0 0 0
3 Russia 0 0 0
4 South Korea 0 0 0



KOMBE LA DUNIA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo

JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Switzerland 2 Ecuador 1
E
Nacional
2200
France 3 Honduras 0
E
Estadio Beira-Rio
0100
Argentina 2 Bosnia 1
F
Estadio do Maracanã
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Germany v Portugal
G
Arena Fonte Nova
2200
Iran v Nigeria
F
Arena da Baixada
0100
Ghana v United States
G
Estadio das Dunas


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad