SANAA ZISIZOFATA MAADILI:-Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Shilole na Ney wa Mitego wapewa Onyo na Serikali…’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 05, 2014

SANAA ZISIZOFATA MAADILI:-Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Shilole na Ney wa Mitego wapewa Onyo na Serikali…’’


Shilole ambaye ni mmoja wa ‘Wasanii waliopewa Onyo na Serikali kuhusu kufanya sanaa ambazo hazifati maadili’.

.....Ney wa Mitego......


........Wema Wema na Aunt Ezekiel......


Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo ,Bw.Juma Nkamia akiwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda Bungeni mjini Dodoma.


Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo ,Bw.Juma Nkamia akijibu swali la Catherine Magige kuhusiana na udhalilishaji wa Wanawake unaofanywa kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania…Waziri Nkamia alisema ‘nakubalia kabisa kwamba kumbi za starehe zimekua zikitoa burudani na ajira kwa vijana hapa nchini lakini ndani ya kumbi hizo kumekua na vitendo vinavyofanyika kinyume na maadili ikiwemo udhalilishaji wa Wanawake’

‘Katika kukomesha hali hiyo serikali kupitia baraza la sanaa BASATA wamefanya vikao kadhaa na wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni, wakuu wa polisi, wamiliki wa kumbi na wanaojihusisha na uchezeshaji wa mtindo wa kanga moja ili kujadili ukiukwaji wa maadili kwenye sanaa’.

Waziri anasema ‘Pia serikali imeacha kutoa usajili kwa vikundi kama cha kanga moko kwa kuwa uchezaji wake unakwenda kinyume na maadili ya Tanzania na kutoa onyo kwa wamiliki wa kumbi, Wasanii na hata asasi zinazojihusisha na sanaa ambazo hazifati maadili’.

Anasema ‘Wasanii waliopewa Onyo ni Ney wa Mitego, Shilole, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na kwa upande wa kumbi ni Mama’s and Papa’s lakini pia maonyesho ya urembo ya Miss Utalii yalifungiwa ambapo pia Serikali imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake/Wasichana watoto’
  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad