PICHA:-Alivyoagwa Director George Tyson Leaders Dar es Salaam June 04,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 05, 2014

PICHA:-Alivyoagwa Director George Tyson Leaders Dar es Salaam June 04,2014.


Wananchi,wasanii pamoja na viongozi mbalimbali wametoa heshima zao za mwisho kwa aliyekua muongozaji wa filamu na vipindi mbalimbali vya televisheni kwa George Tyson ambaye kaagwa June 04, 2014,katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.


Miongoni mwa viongozi waliokusanyika katika kutoa heshima zao za mwisho ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick,baada ya kutoa heshima za mwisho ilifatiwa na kufunika jeneza kwa mbao kisha kupelekwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea Kenya.

Director George Tyson ambaye alizaliwa March 23,1971 amefariki May 30,2014, mkoani Morogoro kwa ajali ya Gari na anategemewa kuzikwa kwao Kenya Jumamosi June 14,Rest in Peace George Tyson.

Hizi ni  baadhi ya picha za Leaders kwenye hatua ya kuaga mwili wa George Tyson.
 

Mike Sangu pamoja na Bakari Makuka wakiwa wamebeba jeneza hilo pamoja na wanakamati wengine.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiaga mwili wa marehemu George Otieno 'Tyson' katika Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam June 04,2014.


Mwigizaji mkongwe, Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' naye akipita kuaga mwili huo.




........Muigizaji Jacob Steven 'JB' akiaga.........


Mke wa muigizaji Kulwa Kikumba 'Dude' naye alikuwepo katika kuaga.


Komedian kutoka mkoani Tanga anayejulikana kwa jina la Mwened naye alishiriki tukio la kuaga mwili wa marehemu Tyson June 04,2014.


...............Muigizaji Hashim Kambi naye akiaga........


.......Thea akiwa anaaga mwili wa marehemu Tyson.....


Ndugu wa marehemu Tyson nao wakipita kumuaga ndugu yao.



.....Monalisa akisaidiwa na watu baada ya kupita kuaga mwili wa marehemu mumewe.......


Mtoto wa marehemu Tyson anayejulikana kwa jina la Sonia akiongea neno kuhusiana na msiba wa baba yake.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akihutubia msibani hapo huku wanahabari wakiwa bize kupiga picha.

Wafanyakazi wa TV1 ambao walikuwa wakifanya kazi na marehemu Tyson wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa kumuaga mfanyakazi mwenzao katika Viwanja vya Leaders ,Dar es Salaam June 04,2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad