Kitendo
hicho kilielezwa kuwa ni kuwazuia waandishi wa habari kutuma taarifa za ajali
hiyo kwenye vyombo vyao vya habari.
Mzozo mkali uliibuka kwa waandishi wa habari
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kituo cha Televisheni cha ITV na Redio
One na mwandishi wa Redio Standard waliokuwa kwenye msafara huo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, (SACP), Geofrey Kamwela alipotafutwa ili aelezee tukio,
alisema hana taarifa kamili na kutaka apewe muda ili afutilie suala hilo aeleze
ajali hiyo.
Hata hivyo baadaye alipotafutwa jioni alisema kuwa
atatolea taarifa suala hilo leo.
Ajali hiyo
iliyohusisha magari matatu ilitokea katika Kijiji cha Kirumbi, Wilaya ya Sikonge,
mpakani mwa mikoa ya Tabora na Singida ikiwa ni siku ya kwanza ya mbio za
Mwenge huo ulioingia mkoani Singida ukitokea Mkoa wa Mbeya.
Mashuhuda wa
ajali hiyo, walisema kuwa ilitokea muda mfupi baada ya Mwenge kupokewa katika
Kijiji cha Rungwa kilichopo Kata na Tarafa ya Itigi.
Ilielezwa kuwa gari moja
la polisi lililokuwa kwenye msafara lilipasuka gurudumu na kusimama pembeni mwa
barabara.
Gari jingine
la polisi lililokuwa kwenye msafara lilisimama ghafla kutaka kufahamu
kilichowapata wenzao, ndipo gari la Ofisi ya Afya ya Mkoa likiwa na wahudumu wa
afya, lililigonga kwa nyuma gari hilo.
Kwa kuwa
kila gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi ili kuendana na gari la Mwenge
lililokuwa limetangulia, gari jingine lililokuwa na askari waliokuwa
wamening’inia juu nalo lililigonga gari hilo la afya kwa nyuma na kusababisha
askari hao kuumia.
Katika tukio
hilo, hakuna hata mmoja kati ya wahudumu wa afya aliyeumia, lakini ajali hiyo
ilisababisha askari mmoja kuvunjika mguu, mwingine kuvunjika mkono huku wawili
hali zao zikiwa nzuri na mwingine alikuwa mahututi.
Baada ya
tukio hilo, waliwahishwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Gasper iliyopo
Itigi kwa matibabu zaidi.
Habari Na:-Mwananchi.
No comments:
Post a Comment