Hakuna matengenezo pale uharibifu unapotokea na Hakuna milango imara kwa ajili
ya kujisitiri.
|
Choo si sehemu inayopewa kipaumbele na huchukuliwa kama sehemu chafu
hivyo huwekwa mbali na makazi.
|
Hakuna milango kwa ajili ya kujisitiri, hakuna dawa wala usafi na huwa siyo suala
la msingi na la kuzingatiwa ni hali ya vyoo kwa baadhi ya shule zetu hapa nchini Tanzania.
|
Waziri wa Wizara ya Afya
Ustawi wa Jamii wa Tanzania ,Dkt. Seif Rashid.
|
WAZIRI wa Wizara ya Afya Ustawi
wa Jamii Tanzania,Dkt. Seif Rashid (MB) amesema kwamba Wizara yake ilifanya utafiti
katika Halmashauri 112 nchini mwaka 2013 ambapo matokeo yanaonyesha asilimia 25
tu ya Kaya kutumia vyoo bora.
Dkt. Rashidi
alisema hayo jana wakati wa kilele cha Siku ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani
yaliyofanyika jijini Mwanza kitaifa, ambapo utafiti huo matokeo yake
yanaonyesha kuwa ni asilimia 29.6 hazina vyoo kabisa huku asilimia 9
kuna vifaa maalum kwa ajili ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kubwa kwa
afya kutokana na wananchi wengi kuwa na mwitikio mdogo wa kujenga vyoo vya bora
vya kisasa.
“Takwimu
hizo ni kielelezo cha kuwepo kwa magonjwa ya kuhara na vile vile
zinaonysha kuwa bado tupo nyuma ikilinganishwa na lengo la kitaifa
tulilojiwekea la kufikia asilimia 53 ya kaya zenye vyoo bora ifikapo mwaka
2016,”alisema .
Rashidi
alisema pia Wizara hiyo ilizindua Kampeni ya kitaifa ya usafi na
mazingia ya miaka minne iliyozinduliwa na mwaka 2012 iliyolenga
kuwezesha kaya milioni 1,520,000 kupata huduma bora za vyoo nchini ifikapo
mwaka 2015 ambpo hadi sasa kampeni hiyo imefanikisha kaya
312,528 kujenga vyoo bora sawa na asilima 56.4 ya lengo hilo.
Aidha kaya
204, 213 zina vifaa maalumu vya kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kwamba vitongoji 9,120
vimesaini makubaliano ya kuboresha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yao
ikiwa ni utekelezaji wake.
Waziri Dkt.
Rashid alitangaza washindi wa tuzo za mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira
kwa mwaka 2014, kundi la kwanza lilihusisha Halmashauri za Majiji manne ya
Tanga, Mbeya, Mwanza na Dar esalam ambapo Jiji la Mwanza limeibuka kuwa mshindi
kwa asilimia 75 ikiwa ni mara ya tisa mfurulizo, Halmashauri za Mikoa mshindi
ni Manispaa ya Kinondoni ilibuka kwa asilimia 55.7 kwa mshindi mmoja.
Kundi
jingine la tatu lilishirikisha Halmashauri za Manispaa 15 ambapo mshindi wa
kwanza ni Manispaa ya Iringa kwa asilimia71.3, mshindi wa pili Manispaa ya Moshi
kwa asilimia 68.1 na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Manispaa ya Morogoro kwa
asilimia 67, kundi la nne ni Halmashauri za Miji ambapo washindi asilimia zao
kweny mabano kuwa ni Mji wa Njombe (67.1), Kahama (63.2) na Mpanda
(60.2).
Wito wangu
ni kuikumbusha jamii juu ya ungonjwa hatari wa Dengue ambao umetokea mlipuko wa
wagonjwa 1,119 kupatwa na kutokea vifo vya watu wanne, kufatia kuumwa na mbu
aina ya “Aedes” ambaye hupata mazalia katika maeneo ambayo si safi akitolea
mfano vifuu vya nazi , makopo, vyungu vilivyotupwa hovyo, matairi ya magari na
maji ya bafuni hivyo kuwataka kuchukua hatua ya kuweka mazingira katika hali ya
usafi.
No comments:
Post a Comment