![]() |
Askofu Mkuu
wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa
Jumamosi hii-June 07,2014.
|
![]() |
Mbunge wa
jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande
Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi
Mtarajiwa ,Meru.
|
![]() |
Bi ,Harusi
Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua
Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru.
|
Na Dixon
Busagaga wa globu ya Jamii kanda ya kaskazini.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari (CHADEMA) kesho jumamosi June 07,2014,anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

Kwa Mujibu
wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu
wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru
Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.
"Nichukue
tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu
wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu ,
Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja
Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on
entrance!"alisema Nassari.
Nassari
amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina
yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .
No comments:
Post a Comment