Shule za
sekondari wilayani Ngara mkoani Kagera zimetakiwa kuanzisha Mpango wa kuwa na
vijana wa skauti ili kuwajengea ukakamavu, maadili na nidhamu nzuri ikiwa ni
sehemu ya malezi bora.
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu ametoa wito huo kupitia taarifa yake
iliyosomwa na Afisa Tawala wa wilaya hiyo Bw David Mafipa wakati wa Uzinduzi wa
tawi la Skauti katika shule ya sekondari Nyabisindu kata ya Kabanga wilayani
Ngara.
Amesema
iwapo kila mwanafunzi wa Sekondari atakuwa Skauti itasaidia kuimarisha nidhamu
shuleni, kuongeza kiwango cha ufaulu na kukabiliana na mimba kwa wanafunzi.
Mkuu huyo wa
wilaya amesema kumbukumbu zinaonesha kuwa shule ya Sekondari ya Nyabisindu ni
ya pili kwa kuwa na vijana wa Skauti na kwamba shuel ya kwanza ni Shunga
Sekondari ambapo ameiagiza Halmashauri kuhakikisha kila shule ya Sekondari inakuwa
na Skauti.
Habari Na:-RK FM-Ngara.
No comments:
Post a Comment