Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza matumizi ya teknolojia mpya ya Biometric
Voter Registration (BVR), katika maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapigakura
ambayo yatafuta matumizi ya vitambulisho vya kupigia kura vya sasa.
Kwa hatua
hiyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ametangaza kuwa: “Katika kura ya
maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa 2015, mpigakura atatumia kitambulisho
kipya atakachopatiwa na Tume baada ya kuandikishwa upya katika mfumo huu na si
vinginevyo.
Vitambulisho
vilivyotolewa katika uandikishaji na uboreshaji uliopita havitatumika tena.”
Akitangaza
mpango huo mpya Dar es Salaam June 19,2014, Jaji Lubuva alisema Tume hiyo itaanza
maboresho ya daftari hilo kwa watu wote wenye sifa za kupiga kura Septemba
mwaka huu na kukamilisha kabla ya kura ya maoni ya Katiba na Uchaguzi Mkuu
2015.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Tanzania(NEC),
Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
|
BVR ni mfumo
wa kuchukua taarifa za mtu za kibaiolojia hasa alama za vidole.
Mwaka 2004,
NEC ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa
taarifa za wapigakura na uhifadhi wa taarifa za kielektroniki.
Sanjari na
hilo, tume hiyo ilitoa vitambulisho vya wapigakura ambavyo pia vimekuwa
vikitumika kwa shughuli mbalimbali za utambulisho katika maeneo kama benki,
polisi, mahakamani, uhamiaji, ukataji leseni, usajili wa simu na mengineyo.
Jaji Lubuva
alisema katika kazi hiyo ya uandikishaji, NEC imekusudia kutumia Sh.293 bilioni
kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, mafunzo ya watendaji na uandikishaji.
Maofisa
watakaotumika katika uandikishaji ni pamoja na waratibu wa uandikishaji wa
mkoa, maofisa waandikishaji ambao watakuwa ni wakurugenzi wa halmashauri,
maofisa wasaidizi watakaokuwa watatu kwa kila jimbo, watendaji kata na waratibu
wa elimu.
Mafunzo kwa
watendaji hao yanatarajiwa kuanza Julai, 2014 na uandikishaji utaanza Septemba
na katika vituo 40,015 kote nchini.
Jaji Lubuva
alisema kwa utaratibu wa sasa, vituo vya kujiandikishia vimeongezeka kutoka
24,919 hadi 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za vitongoji, vijiji na mitaa
ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.
Mfumo BVR
uliwahi kutumika katika nchi mbalimbali na kuripotiwa kushindwa kukamilisha
shughuli hiyo kutokana na sababu kadhaa za kiufundi au ukosefu wa umeme.
Tanzania
haitakuwa ya kwanza kuutumia kwani ulishatumiwa na nchi za Nigeria 2007, Ghana
2009, Liberia 2005, Guinea 2005, Mali 2005, Uganda 2008, Kenya 2013, Zambia
2008, Afrika Kusini na Zanzibar 2009.
Chanzo:-Mwananchi.
No comments:
Post a Comment