MANISPAA BUKOBA:-Baada ya Madiwani sita kutimuliwa,angalia kilichotokea Mahakamani –June 20,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 21, 2014

MANISPAA BUKOBA:-Baada ya Madiwani sita kutimuliwa,angalia kilichotokea Mahakamani –June 20,2014.

Baadhi ya wananchi wakitoka nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Kagera ambayo imewavua nyadhifa za udiwani madiwani 6 kati ya 8 waliokuwa wakishitakiwa kwa kosa la kushindwa kuhudhuria vikao vya Kikanuni vya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo madiwani hao hawajahudhuria vikao vilivyoitishwa July 19, August Mosi, September 23, November 11 na Novemba 14 mwaka jana.

Dk Anatory Aman akipongezana na Wakili Aaron Kabunga aliyesimamia kesi iliyofunguliwa na Chifu Kalumuna na hatimaye madiwani sita kutimuliwa ambapo Madiwani walalamikiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Diwani Yusuph Ngaiza (Kashai -CCM), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo -CCM), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo -CCM) na Deusdedith Mutakyahwa wa Kata ya Nyanga -CCM.

 Wengine ni Richard Gaspar (Miembeni -CCM), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu CCM), Israel Mulaki (Kibeta -CHADEMA) na Rabia Badru (Viti Maalumu -CUF).
 


Mulungi Kichwabuta naye akiendesha gari kuondoka mahakamani baada ya hukumu ambapo naye pia ni miongoni mwa madiwani sita.

Diwani Yusuph Ngaiza na Mwenekiti wa CCM Manispaa ya Bukoba akiendesha gari kuondoka eneo la Mahakama akiwa ni miongoni mwa waliovuliwa udiwani kwa kupoteza sifa.


Huyu haikujulikana kama alikuwa anashangilia matokeo ya hukumu……Picha Na:-Harakatinews Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad