Zaidi ya wanaume elfu 4 na
mia 6 wamefanyiwa tohara katika Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara wakati wa
zoezi linaloendeshwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia ofisi ya
Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera.
Mratibu wa zoezi hilo Bi Merisa
Lutayabulwa amesema hayo wakati akizungumza na Radio Kwizera kuhusu
Mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa zoezi la la tohara kwa Wanaume
lililoanza May 19,2014 hadi June 05,Mwaka huu kabla ya kuhamia katika Zahanati ya Mukatabo katika kata ya Kirushya wilayani Ngara.
Bi Lutayabulwa amesema licha
ya wanaume wengi kujitokeza kupata huduma hiyo lakini changamoto kadhaa
zimejitokeza ikiwemo baadhi ya watu kurudi tena hospitali wakiwa wanavuja damu
kutokana kushindwa kufuata maelekezo waliyopewa awali baada ya kufanyiwa tohara.
Habari Na:-Radio Kwizera
FM-Ngara.
No comments:
Post a Comment