MAJONZI:-Mamia wamzika Msanii Mkongwe wa Maigizo nchini Tanzania Said Ngamba-Mzee Small katika makaburi ya Segerea Dar es Salaam-June 09,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 10, 2014

MAJONZI:-Mamia wamzika Msanii Mkongwe wa Maigizo nchini Tanzania Said Ngamba-Mzee Small katika makaburi ya Segerea Dar es Salaam-June 09,2014.

Msafara wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwa ajili ya Kumpumzisha Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu Mzee Small June 09,2014.

Nguli wa michezo ya kuigiza na vichekesho, Saidi Wangamba ‘Mzee Small’ (59), amefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam akiwa ni msanii wanne kukutwa na mauti katika mwezi mmoja.

Kifo cha msanii huyo ambaye amezikwa June 09,2014 katika Makaburi ya Segerea, Dar es Salaam  kimetokana na ugonjwa wa kiharusi uliompata, mwaka 2012 alipoanguka bafuni na baadaye kupooza upande wa kushoto.

Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza) likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye Makaburi ya Segerea jioni Hii.

 Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea. 


Vijana wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small june 09,2014.

Vijana wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small wakielekea kwenye Makaburi ya Segerea  jana June 09,2014 Jioni .



Mwili wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.


Watu mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika Mzee Small June 09,2014. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad