HABARI/PICHA:-Tazama Joka kubwa aina ya Chatu lilivyouawa Na wananchi Eneo la Sakina mkoani Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 06, 2014

HABARI/PICHA:-Tazama Joka kubwa aina ya Chatu lilivyouawa Na wananchi Eneo la Sakina mkoani Arusha.


Chatu huyo akiwa ametumbukia ndani ya nyumba Hiyo maeneo ya sakina mkoani Arusha.


Kwa mujibu wa Arusha yetu Blog wanasema kuwa Chatu huyo aliuwawa na wananchi mchana wa June 05 na ni baada ya kuonekana  maeneo ya Sakina Arusha akiwa amefungwa kitambaa chenye maaandishi mekundu.
 
Wakazi wa eneo la Sakina wamepatwa na mshtuko mkubwa,kikubwa zaidi kwa Chatu huyo ni kuwa inasemekana alionekana akiingia ndani.

Mara baada ya kuonekana kwa Chatu huyo wananchi walijipanga kisha wakafanikiwa kumuua ingawa kulitokea utata baada ya Mama mwenye nyumba aliyetokea Chatu huyo kupinga kuuliwa kwa Chatu huyo,Chatu huyo aliuwawa kisha akakatwa vipande vipande.


Kwa mbaliii nikitambaa ambacho alikuwa amefungwa chatu huyo  ambapo Wakazi wa eneo la Sakina mkoani Arusha June 05,2014 walipatwa na mshtuko mkubwa bada ya kuona chatu akiwa anaingia ndani ya nyuma ya jirani yao huku akiwa amefungwa kitambaa kilichokuwa na maandishi mekundu yasiyoeleweka mkiani mwake…

.Ndipo wakazi hao wakaanza kumvizia chatu huyo na kutaka kumpiga lakini utata ukaibuka baada ya kudaiwa mama mwenye nyumba hiyo kusema wasimuue kwani ni mtoto wake,Lakini majirani hao hawakukubali ndipo walimkamata na kumuua kwa kumkata kata viapande.


 Hicho ni kitambaa ambacho alikuwa amefungwa chatu huyo kwa nyuma kikiwa kina maandishi mekundu.


Chatu akiwa anatamba pembeni ya ukuta kuingia ndani ya nyumba lakini Wananchi walifanikiwa kumuua ,tukio likitokea june 05,2014, maeneo ya sakina mkoani Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad