![]() |
……….Moja
ya aina za sumu ya panya....Picha Na:-Maktaba Yetu...... |
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Andrew Kabuka, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw George Gorotho amemtaja Msichana huyo kuwa ni Rosemary Masaru mkazi wa Musoma mjini mkoani Mara.
Bw Gorotho ameiambia Mahakama
kuwa mshitakiwa huyo anadaiwa kutaka kujiua katika tukio la May 28,mwaka huu,majira
ya saa 7 mchana katika shule ya Sekondari ya Ntobeye ,jambo ambalo ni kinyume
cha sheria.
Mtuhumiwa amekana shitaka
linalomkabili na yuko nje kwa dhamana
ya Sh laki 5 baada ya kutimiza
masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na mdhamini ambaye ni mtumishi wa serikali
na mkazi wa wilaya ya Ngara ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi June 17 mwaka huu.
Katika hatua Nyingine, Mwanafunzi mwenye umri wa
miaka 17 anayesoma katika shule ya Sekondari Kanazi wilayani Ngara,mkoani Kagera amehukumiwa
na Mahakama ya wilaya hiyo kutumikia adhabu ya kuchapwa viboko 9 baada ya
kumkuta na na makosa mawili ambayo ni ubakaji na kusababisha ujauzito
Mbele ya hakimu wa wilaya ya
Ngara Bi Mariam Rusewa, Mwendesha mashitaka wa Polisi ,Bw Tumaini Membi amemtaja
mshitakiwa kuwa ni Jady Miburo mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa
Mukirehe wilayani Ngara
Habari na :-Radio Kwizera FM.-Ngara
No comments:
Post a Comment