MSIBA WA MTOTO WA BOKSI :-Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro wajitokeza kuuaga Mwili wa Mtoto Nasra na kuzikwa leo June 3, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 03, 2014

MSIBA WA MTOTO WA BOKSI :-Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro wajitokeza kuuaga Mwili wa Mtoto Nasra na kuzikwa leo June 3, 2014.

Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliojitokeza Kuuga Mwili wa mtot Nasra ambapo….Historia ya Nasra……..

Nasra aligundulika akiwa amefichwa katika boksi na mama yake mkubwa, Mariam Said huko Uwanja wa Ndege, Morogoro ikielezwa kuwa alikuwa humo tangu akiwa na umri wa miezi tisa alipomchukua kumlea baada ya mdogo wake (Mama Nasra), kufariki dunia.

Akiwa ndani ya boksi hilo ilidaiwa kuwa alikuwa akiwekewa chakula huku akijisaidia na kulala humohumo hali iliyosababisha atapakae kinyesi mwili mzima.
Mariam na mumewe, Mtonga Ali (30) na Mvungi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Morogoro kujibu mashtaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

 Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi leo June 3, 2014.
 
Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra Rashid (4) likiwa katika uwanja wa Jamhuri mkoa wa Morogoro kabla ya mazishi yake katika makaburi ya Kola mkoani humo leo June 3, 2014.

 ....Mwili wa mtoto Nasra ukipelekwa makaburini Kuzikwa…
 Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa Marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.
 

......Waombolezaji wakiingia katika mabasi ya Abood, kwenda katika maziko......
Mazishi ya mtoto Nasra yamefanyika katika  makaburi ya Kola mkoani Morogoro leo June 3, 2014.



Mbunge Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.


Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu leo June 03,2014.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad