KOMBE LA DUNIA 2014:-Uswisi yaifumua Ecuador 2-1 .. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 15, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Uswisi yaifumua Ecuador 2-1 ..


Winga wa Ecuador, Antonio Valencia akiwa a einua mguu juu kupiga mpira dhidi ya beki wa kushoto wa Uswsi, Ricardo Rodriguez.

Timu ya Taifa ya ECUADOR, wakiongozwa na Staa wa Manchester United Antonio Valencia Usiku wa June 15, 2014, wamelimwaga baada kuongoza Bao 1-0 na kuiruhusu Uswisi kuwafunga 2-1 katika Mechi yao ya Kwanza ya Kundi E la Fainali za Kombe la Dunia kwenye Mechi iliyochezwa huko Estadio Nacional Mjini Brasilia.



Kitu cha kusikitisha mno kwa Ecuador ni kuwa kwenye Dakika ya 92, huku Bango likiwa tayari limeashiria Dakika 3 za Nyongeza, Antonio Valencia alichanja mbuga na kuingia ndani ya Boksi na kumpa Pasi murua Arroyo amalizie tu lakini Mchezaji huyo alifanya mbwembwe na Mpira kunaswa na Behrami na Uswisi kuanza shambulizi lao la nguvu ambalo walifunga Bao lao la ushindi.
Bao hilo lilifungwa na Haris Seferovic kwenye Dakika ya 92 na Sekunde 41.
KOMBE LA DUNIA 2014.
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo.

JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Switzerland 2 Ecuador 1 E Nacional
2200 France v Honduras E Estadio Beira-Rio
0100 Argentina v Bosnia F Estadio do Maracanã
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Germany v Portugal G Arena Fonte Nova
2200 Iran v Nigeria F Arena da Baixada
0100 Ghana v United States G Estadio das Dunas



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad