KOMBE LA DUNIA 2014:-Kufungwa Italia 1-0 na Costa Rica,Uingereza kufuzu 16 Bora ni ndoto huku Ufaransa ikishinda 5-2 Switzerland. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 21, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Kufungwa Italia 1-0 na Costa Rica,Uingereza kufuzu 16 Bora ni ndoto huku Ufaransa ikishinda 5-2 Switzerland.

Giroud & Matuidi both score in 66 seconds for France-June 20,2014-Timu ya Taifa ya Ufaransa imejikatia tketi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora ya Fainali za Kombe la Dunia 2014-Brazil, ikiongoza kundi E licha ya kuwa na mechi moja imesalia dhidi ya Equador iliyoshinda 2-1 dhidi ya Honduras.

Switzerland imebakia ya pili ikiwa na alama tatu na hivyo hainabudi kushinda mechi yao ijayo dhidi ya honduras kujihakikishia nafasi katika 16 bora.

Timu hiyo ya Ufaransa iliyoishinda Honduras 3-0, katika mechi yao ya ufunguzi, iliitandika timu ya Uswisi iliyokua na sifa ya kutoshindwa katika michuano kumi, ya kombe la dunia,kwa Olivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya kumi na saba naye Blaise Matuidi akafunga la pili sekunde chache baadaye,Karim Benzema alipewa penalti lakini mkwaju wake ukazuiwa na kipa wa Uswisi, Diego Benaglio.

Yohan Cabaye aliurudisha mpira baada ya kuokolewa na Benaglio, ila uligonga juu ya lango la Uswisi.Ufaransa waliongeza bao la tatu kabla ya muda wa mapumziko.

Olivier Giroud alimpa Mathieu Valbuena pasi safi baada ya kona ya waswisi.Valbuena hakupoteza nafasi hiyo na akautia mpira kwenye wavu wa timu ya Uswisi.

Katika dakika ya 67, Benzema alikosoa kosa lake la kutofunga penalti kwa kufunga bao lingine baada ya kupokea pasi kutoka kwa Paul Pogba.

Hilo likawa bao la nne bila jibu kwa timu ya Ufaransa huku Kisha Benzema akachangia katika kufunga la tano kwa kumpa Moussa Sissoko pasi ambayo Sissoko alitia wavuni.

Katika dakika za mwisho, timu ya Uswisi ilifanikiwa kupata mabao ya kufutia chozi hata ingawa hayakua na uwezo wa kurekebisha matokeo ya mchuano huo.

Blerim Dzemaili alipiga mkwaju wa adhabu uliopita safu ya ngome ya Les Bleusna kuingia na Ufaransa kushinda mchezo kwa bao 5-2.
 
Mario Balotelli alikosa mabao mawili ya wazi katika mchezo huo wa Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia June 20,2014 wakati Matumaini ya Timu ya Taifa ya Uingereza kufuzu 16 Bora ya Kombe la Dunia yakiyeyuka baada ya Costa Rica kuifunga Italia 1-0.

Haya ni matokeo mabaya zaidi kwao tangu mwaka 1958 wakifungwa mechi mbili za mwanzo na Italia na Uruguay, ambao sasa watatoana jasho katika mchezo wa mwisho kuwania kuungana na Costa Rica kutoka kundi hilo kwenda Raundi ya Pili.

Bao pekee la mchezaji Bryan Ruiz dakika ya 44 ndilo limeizamisha Italia, ambayo nayo sasa iko mguu nje, mguu ndani kwenye fainali za mwaka huu.

Uingereza itamaliza na vinara wa kundi hilo, Costa Rica waliozitoa nishai Italia na Uruguay, ikiwa tayari imeaga. 

IJUMAA, JUNI 20, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Italy 0 v 1 Costa Rica
D
Arena Pernambuco
2200
Switzerland 2 v 5 France
E
Arena Fonte Nova
0100
Honduras 1 v 2 Ecuador
E
Arena da Baixada
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina v Iran
F
Estadio Mineirão
2200
Germany v Ghana
G
Estadio Castelão
0100
Nigeria v Bosnia-Herzegovina
F
Arena Pantanal
JUMAPILI, JUNI 22, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium v Russia
H
Estadio do Maracanã
2200
South Korea v Algeria
H
Estadio Beira-Rio
0100
United States v Portugal
G
Arena Amazonia

As It Stood Table FIFA World Cup 2014.

Position Team Played Goal Difference Points
1 Brazil 2 2 4
2 Mexico 2 1 4
3 Croatia 2 2 3
4 Cameroon 2 -5 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Netherlands 2 5 6
2 Chile 2 4 6
3 Australia 2 -3 0
4 Spain 2 -6 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Colombia 2 4 6
2 Ivory Coast 2 0 3
3 Japan 2 -1 1
4 Greece 2 -3 1

Position Team Played Goal Difference Points
1 Costa Rica 2 3 6
2 Italy 2 0 3
3 Uruguay 2 -1 3
4 England 2 -2 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 France 2 6 6
2 Switzerland 2 -2 3
3 Ecuador 1 0 3
4 Honduras 1 -4 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Argentina 1 1 3
2 Iran 1 0 1
3 Nigeria 1 0 1
4 Bos-Herce 1 -1 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Germany 1 4 3
2 USA 1 1 3
3 Ghana 1 -1 0
4 Portugal 1 -4 0

Position Team Played Goal Difference Points
1 Belgium 1 1 3
2 Russia 1 0 1
3 South Korea 1 0 1
4 Algeria 1 -1 0



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad