Mchezo wa
ufunguzi ulichezwa usiku wa June 12, 2014, Kwa wenyeji Brazil dhidi ya Croatia
ikiwa ni mchezo wa Kundi A na matokeo ni wenyeji Brazil wakianza vyema Fainali
za Kombe la Dunia 2014 kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Croatia kwenye uwanja wa
Corinthias, mjini Sao Paulo.
Croatia waliotawala sehemu ya kiungo, waliuanza vizuri mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 11 ya mchezo huo baaada ya beki wa Brazil Marcelo kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa.
Magoli ya
Brazil yamefungwa na Neymar, aliyefunga mawili kwa Penati dakika ya 29 na 71,
Oscar nae kuongeza bao la 3 dakika ya 90.
Michuano hiyo itaendelea tena June 13, 2014, saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Mexico dhidi ya wawakilishi wa Afrika ,Cameroon huku Mabingwa watetezi Hispania wakicheza na Uholanzi saa Nne usiku kasha Chile dhidi ya Australia saa Saba usiku.
Neymar
akimfunga kwa penalty kipa Stipe Pletikosa wa Croatia aliyekaribia kuokoa
mkwaju huo kama si kuupangulia nyavuni kwake.
|
No comments:
Post a Comment