Gari la Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka likiwa katika kituo cha polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kugonga punda June 11,2014. |
Walioshuhudia
tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo gari lenye namba za usajili STK 5857mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42)
liligonga mnyama punda aliyekatiza ghafla barabarani.
Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyang'a,Bw Benson Mpesya
amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa Waziri Tibaijuka alipata
mshtuko baada ya ajali hiyo na ofisi ya mkuu wa wilaya Kahama ilimpatia usafiri
mwingine kwa ajili ya kuendelea na safari ili kuhudhuria vikao vya bunge
kufuatia gari lake kuharibika.
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka |
Hata hivyo
mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema waziri
Tibaijuka hakuumia katika ajali hiyo na leo ameendelea na vikao vya bunge
mkoani Dodoma.
Akielezea zaidi kuhusu ajali hiyo ,Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya amesema Waziri Tibaijuka alikuwa na
baadhi ya wanafamilia wake katika gari hilo wakitoka Bukoba kwenda Dodoma kwa
ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea.
Kamanda
Kihenya amesema baada ya kufika katika eneo hilo alikatisha punda
katikati ya barabara na katika harakati za dereva kumkwepa ndipo gari hilo
lilipomgonga na kisha mnyama huyo kufa papo hapo.
Kihenya
alisema kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia ila kuna baadhi ya watu
waliopata majeraha madogo madogo ikiwa ni pamoja na waziri huyo aliyepata
mshtuko kidogo lakini baadaye hali yake iliendelea vizuri.
Hata hivyo katika hali ya mshangao wa watu
waliomiminika katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kumjulia hali
waziri na kumpa pole lakini Waziri huyo na msafara wake walikuwa wakipatiwa
matibabu na wauguzi katika Hoteli moja iliyopo pembeni mwa hospitali ya Wilaya
Kahama.
No comments:
Post a Comment