Binti huyo,
mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa
akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa
Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa
katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada
namba OB/RB/9967/2014.
![]() |
Yusta Lucas (20). |
Akisimulia
masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta
alisema: ...“Nililetwa Dar es Salaam mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya
bosi wangu (Amina) ambaye ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba
nije kumsaidia kazi ndogondogo.”
Alisema
aliishi vizuri na mwajiri wake huyo, lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza
kubadilika akidai kuwa Amina alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa
pasi kila alipomtuhumu kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa
akinichapa na kuning’ata sehemu mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma
kwa pasi yenye moto kila aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”
Hakuwahi
kupelekwa Hospitali.
Alisema
licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu hizo, mwajiri wake huyo hakuwahi
kumpeleka hospitali na pale alipoona hali ni mbaya alimnunulia dawa...
“Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka mumewe na mtoto wake kumpeleka shule ya
bweni... niliugulia hadi nikapona bila mtu mwingine kufahamu.”
“Akienda
kazini anafunga geti na kunikataza kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni
nilikuwa naenda siku ambazo yeye yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na
kurudi pasipo kuzungumza na mtu yeyote.”
Alisema
mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za mshahara wake kwa mama yake akisema
ndiye anayepaswa kulipwa, jambo ambalo anadhani limemfanya mama yake kuhisi
mwanaye yuko katika mikono salama... “Kila alipotuma alipiga simu na kunipa
niongee na mama kuhakikisha kama zimefika huku akinisimamia na baada ya hapo
anachukua simu.”
Ataka kurudi
kwao.
Binti huyo
ambaye sehemu kubwa ya mwili wake ina alama za kung’atwa meno na majeraha ya
kuchomwa na pasi, alisema: “Ninaomba mtu yeyote mwenye hela, nataka nikitoka
hapa hospitali nirudi Tabora kwa mama.
Nina shaka na maisha yangu hapa kwa huyu
mama… sitaki tena kubaki Dar es Salaam kutokana na mateso ninayoyapata.
Polisi
wasema.
Mkaguzi
Msaidizi wa Dawati la Jinsia Polisi Mkoa wa Kinondoni, Prisca Komba alisema
taarifa za binti huyo ziliwafikia baada ya majirani kupeleka taarifa hizo
katika Kikundi cha Kipange kilichopo Kwa Manjunju ambacho nacho kilitoa taarifa
polisi na ndipo mtego wa kumnasa mwanamke huyo ukawekwa.
Majirani
walichukua hatua hiyo kutokana na kusikia kelele za kilio mara kwa mara zikitokea
ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.
“Tumekagua makovu na majeraha mbalimbali yaliyo
katika mwili wake na kupata jumla kuwa yako 91,” alisema Komba.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Thobias Edoyeka alisema suala hilo
linashughulikiwa na polisi pamoja na ustawi wa jamii, kauli iliyoungwa mkono na
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mwananyamala, Rose Temu ambaye alisema wanafuatilia
kwa karibu matibabu yake pamoja na usalama wake.
Ofisa
Muuguzi Msaidizi Wodi Namba Tatu ambayo ni ya kinamama, Rose Mussa alisema
Yusta anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment