........Waziri wa
Fedha, Saada Salum Mkuya..........
|
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya aliposoma Hotuba ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Alisema hayo
mjini hapa juzi, wakati akielezea matumizi ya fedha kwa makundi maalumu, hasa
kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu.
Waziri huyo alisema serikali inaendelea na
utaratibu wa ujenzi wa nyumba za walimu kwa awamu.
Alisema
katika mwaka wa fedha 2013/14, halmashauri 40 zilipewa kila moja Sh milioni 500
ili zianze ujenzi wa nyumba za walimu. Kiasi kama hicho, kitatolewa katika
halmashauri hizo kwa mwaka 2014/15.
“Aidha, Sh
milioni 500 zitatolewa kwa halmashauri 80 zaidi, hivyo kufanya jumla ya
halmashauri 120 kunufaika na utaratibu huo, lengo likiwa ni kuzifikia
halmashauri zote mwaka 2015/16”, alisema.
Aliwahimiza
viongozi wa Serikali katika ngazi za mikoa, wilaya na kata, kusimamia
kikamilifu fedha hizo ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kuhusu
malipo ya madai ya walimu, alisema serikali inaendelea kulipa madai ya walimu
yaliyohakikiwa, ambapo katika mwaka 2014/15 kiasi cha Sh bilioni 5.6 kimelipwa.
“Aidha, kwa
mwaka 2014/15 madai ya walimu ambayo yatakuwa yamehakikiwa, yataendelea
kulipwa.
Aidha,
Waziri huyo alisema uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi,
umeimarishwa kutoka 1:47 mwaka 2012 na kufikia 1:43 mwaka 2013, ikilinganishwa
na lengo la uwiano wa 1:40.
Katika elimu
ya sekondari, uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi ulifikia lengo la MKUKUTA II la
1:28 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment