Rais Kenyatta akigawa tiketi kwa wachezaji huku akishuhudiwa na mkewe Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto). |
......Rais Kenyatta akiongea na wachezaji wa Harambee Stars.........
|
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya
soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia
Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil.
Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil.
Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji
wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa
moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika
baadaye mwakani.
Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais
Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao.
Rais atagharamia tiketi za timu hiyo
kutazama michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi
watakazotazama.
Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa
kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa
wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya.
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili
vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini.
Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini
na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.
Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao
kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil. Ufadhili huu unakuja miezi sita
baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja
miotano ijayo.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii
kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu
kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili
na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.
BBC
No comments:
Post a Comment