AJALI:-Soma kilichosababisha Ajali ya Basi la New Force ,ikiua watu 2 na wengine 40 Kujeruhiwa mkoani Mbeya June 18,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 19, 2014

AJALI:-Soma kilichosababisha Ajali ya Basi la New Force ,ikiua watu 2 na wengine 40 Kujeruhiwa mkoani Mbeya June 18,2014.

Hivi ndivyo basi la New Force linavyo onekana kwa Mbele Baada ya kupata ajali jana June 18,2014 baada ya kupata Ajali ambapo Basi hilo lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda mkoani Mbeya na limepata Ajali eneo la Igurusi na kusababisha Vifo vya watu wawili Papo hapo na kujeruhi wengine Arobaini(40) ambao wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akiwa anatembelea eneo ambapo ajali hiyo ilitokea.

Askari wa Usalama wa barabarani wakiwa eneo la tukio.

 …………Basi la New Force upande wa Mbele lilivyoharibika baada ya kupata ajali jana June 18,2014…

Miili ya watu wawili waliofariki katika ajali hiyo na walikuwa ni watembea kwa miguu.




Mashuhuda katika ajali hiyo wakifatilia kilichokuwa kikiendelea.
Basi la New Force lenye namba za Usajili T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.


WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954 AMH AINA YA  FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. 

PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. 

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI, AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. 

AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad