MWENGE WA UHURU 2014 MKOANI KAGERA:-Picha ya Miradi saba iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru,wilayani Ngara mkoani Kagera-Mei 08,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 08, 2014

MWENGE WA UHURU 2014 MKOANI KAGERA:-Picha ya Miradi saba iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru,wilayani Ngara mkoani Kagera-Mei 08,2014.


Mwenge wa Uhuru 2014, umekabidhiwa kutoka wilayani Karagwe na mkuu wa wilaya hiyo  Dary Rwegasira aliukabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu eneo la Benako kata ya Kasulu wilayani Ngara majira ya saa 2 asubuhi ya leo Mei 08,2014.


Mara baada ya kuupokea Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Kanyasu(kushoto pichani) alisema ukiwa wilayani kwake Utazindua, Kukagua,Kufungua na Kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya shilingi Bilioni 1 na milioni 213 katika miradi ya sekta ya maji eneo la Benaco, kilimo kwenye shamba la migomba la Samweli Kapalala, Kuzindua Kibanio cha Mifugo Nyakisasa (Tsh 12mil) na kuweka jiwe la msingi Kituo cha Afya kijiji cha Kashinga  kata ya Nyakisasa,Mradi wa hifadhi ya mazingira katika shule ya sekondari Rulenge  ambayo imepanda miti iliyopo sasa milioni 12 na malengo ni kufikisha miti milioni 30, ambapo kila Mwanafunzi hupanda miti 5 kwa kila mwaka pamoja na kuzindua jengo la utawala katika Shule ya sekondari ya Rhec English Medium kata ya Rulenge  na hatimaye kutoa cheki ya mikopo kwa SACCOS ya vijana mjini Ngara

Kaimu kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014,kitaifa Bw.Hamza Muhamudi akikata mkungu wa ndizi katika shamba la  migomba la Bw.Samweli Kapalala (Kulia kwake) katika kijiji cha Kasulo Wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kupewa kama zawadi,Mwenge wa Uhuru umefanya ziara yake leo Mei 08,2014.

Akitoa taarifa za mradi wa shamba hilo Samweli Kapalala  alisema katika shamba hilo  hupanda migomba inayotoa ndizi aina ya Nchakala  na sehemu ya shamba amepanda migomba aina ya FIA 17& 23 kwa kutumia wataalamu wa kilimo na kwamba  mkungu wa ndizi unauzwa kati ya Sh 15,000/-kwa aina ya Nchakala na Sh 35,000/ kwa ndizi aina ya FIA 17& 23 ambapo katika faida aliyokwisha pata ni kusomesha watoto kununua ng’ombe  na amejenga nyumba bora Pamoja na faida hiyo alisema tangu kuanzishwa kwa shamba hilo hadi sasa lina thamani ya Sh. Milioni 250 lakini katika uzalishaji zimeshapatikana Sh. Milioni 375 , ingawa changamoto ni ukosefu wa soko na ugonjwa wa unyanjano. 

Pia uliweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya kijiji cha Kashinga  kata ya Nyakisasa,wilayani Ngara leo Mei 08,2014.
Katika mbio zake wilayani Ngara Mei 08,2014 ,Mwenge wa Uhuru 2014 ulizindua Kibanio cha Mifugo Nyakisasa (kilichojengwa kwa thamani ya Tsh 12mil).

Mkesha wa mwenge umefanyika katika viwanja vya posta ya zamani mjini Ngara na utakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,Bw.Richard Mbeo katika kijiji cha Nyabugombe kata ya Nyakahura Mei 09,2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad