Sehemu ya
vitabu vyenye ripoti hiyo.
|
Ofisi ya
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania-CAG imesema kwamba kitendo
cha Serikali kukosa nyaraka za mali zake kumechangia baadhi ya watendaji wasio
waaminifu kutumia mwanya huo kujisogezea mali za umma.
Katika
ripoti yake ya Ukaguzi kwa mwaka 2013- CAG, Ludovick Utouh amesema ofisi yake
imebaini upotevu wa magari 11 yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi na mamlaka
ya maendeleo na biashara Tanzania (TanTrade) ambayo hadi sasa hayafahamiki
yalipo.
Ofisi yake
inalifanyia uchunguzi suala hilo na tayari imegundua hayo magari yalisajiliwa
kwa namba binafsi badala ya namba za serikali huku akisema ‘wizara ya viwanda
na biashara ilinunua magari kwa ajili ya bodi ya biashara na tunaomba kusema magari hayo tumejaribu
kuyafatilia lakini hayaonekani na hayajulikani yalipo na ni magari mapya
yalinunuliwa kwa ajili ya TanTrade lakini TanTrade wenyewe wanasema
hawajayapokea na Wizara inasema haijui yako wapi’
Kwenye hatua
nyingine ,Kamati ya kudumu ya Bunge serikali za mitaa LAAC imesikitishwa na
kitendo cha halmashauri ya jiji la Mwanza kupata hati chafu za hesabu kwa mwaka
2013 na kupanga kwenda kufanya uchunguzi juu ya kilichochangia kutokea kwa hiyo
ishu.
Mwenyekiti
wa LAAC ,Bw.Rajabu Mbaruku amesema kamati yake imepata upinzani ilipotaka
kukagua hesabu za halmashauri hiyo baada ya watendaji wake kukimbia ofisi zao
kwa hiyo kamati ikashindwa kufanya mahojiano na ukaguzi katika jiji la Mwanza.
‘Sasa
tutakapoanza shughuli zetu mkoa wa kwanza utakua Mwanza
Spika wa
Bunge ametangaza kupanga ratiba ili kutoa fursa kwa ripoti hiyo ya hesabu za
serikali kwa mwaka ulioshia June 30 2013 kujadiliwa na wabunge.
No comments:
Post a Comment