KUKOPA:-Mtanzania kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111. ..Ni sababu ya Deni la Taifa kupanda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, May 09, 2014

KUKOPA:-Mtanzania kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111. ..Ni sababu ya Deni la Taifa kupanda.



Deni la Taifa limepanda kutoka trilioni 16.98  mwaka wa fedha 2011/2012 hadi kufikia trilioni 21.2, kiwango ambacho kikigawanywa kwa kila Mtanzania kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ameweka hadharani deni hilo  wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni.

Utouh amesema ongezeko hilo limesababishwa na mikopo kutoka kwenye mabenki na nchi wafadhili kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo.

Utouh amesema deni la nje limefikia Sh. trilioni 15 hadi Juni 30, 2013  ambalo ni ongezeko la Sh. trilioni 3.0 kutoka Sh. trilioni 12.43 kwa mwaka 2011/12, wakati lile la ndani limefikia Sh. trilioni 5.78 ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 1.23 kutoka Sh. trilioni 4.55 kwa mwaka 2011/12.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amepongeza ukaguzi huo kubaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kunusuru fedha za walipakodi ambapo amesema kuwa  ripoti hiyo itaanza kufanyiwa kazi kuanzia sasa hadi Novemba ili kutoa maelekezo kwa hatua mbalimbali ambazo serikali itapaswa kuzichukua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad